Wednesday, April 27, 2011

"Demokrasia sio Ghasia"

      Mataifa mengi ya Afrika    yamejikuta yakiingia katika chuki uhasama uadui hadi vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokana na udini ukabila na tofauti za kiitikadi zinazo wapelekea kuzidi kuwa maskini na omba omba kila siku kwa mataifa ya magharibi. 
     Pamoja na hali duni tuliyonayo ya uchumi na teknelojia hafifu bado tunaendelea kuuana sisi kwa sisi  na kuzidi kujirudisha nyuma kimaendeleo kila siku tunagombana sisi tu!
  Pindi tunapata uhuru nchi nyingi za afrika ikiwemo Tanzania tuliongozwa na mfumo wa kisiasa wa chama kimoja (Monoparty) Ila baada ya muda kitambo tulibadili mfumo huo na kuupokea mfumo wa vyama vingi katika siasa, ulopendekezwa na wazungu, 
Nasio kwamba mfumo huo ni mbaya au haufai no!
Ni mfumo mzuri sana wa kuwapa watu fursa zaidi katika kuchagua viongozi wanaowapenda, lengo likiwa ni kuleta changamoto ya utendaji kazi katika serikali kwa ajili ya uongozi bora na maendeleo kwa manufaa yetu sote.    
          Licha ya udhaifu wake Mfumo wa chama kimoja nao ulikuwa na faida kubwa sana kwa watanzania ulitujenga na kutuimarisha kama taifa na undugu miongoni mwetu na kutupa Amani, ushirikiano, upendo na umoja huu uliopo na kudumu hadi leo, Ijapokua ulitubana kidemokrasia kwa kutunyima uwanda mpana katika maamuzi juu ya  serkali inayotuongoza.              
        Kikubwa nachosema ni hiki ; 
                        Watanzania na Afrika nzima kwa ujumla hatuna budi kulitambua hili sisi ni ndugu.
umoja ushirikiano na mshikamano wetu tuliokua nao tusiuharibu!!
kwamba uwepo wa vyama vingi usijenge mgawanyo na makundi miongoni mwetu na kuanza kunyoosheana vidole na kupigana sisi kwa sisi na kuibua matabaka mengine ndani ya taifa moja!
hilo sio lengo.
Leo nchi nyingi za Afrika wanapigana kisa kugombania madaraka , wengine wanadai wanataka demokrasia yaani hawatendewi haki na kuanzisha ghasia na maandamano yanayoondoka na roho za watu wengi! 
ukiwauliza demokrasia jamani demokrasia sio ghasia!!!
mambo yanafanywa kwa mazungumzo na taratibu za kisheria  kisha mabadiliko yanatokea tena kwa amani kabisa na sio kusimaama mbele ya halaiki na kusema kwa hasira na ghadhabu kuwapandia watu chuki na uasi matokeo yake ni kuuana na suluisho lisipatikane!
Serikali sikivu na makini yenye demokrasia ya kweli husikiliza watu wake maana ndio maana ya demokrasia yenyewe kwa kitendo cha serikali kutoridhia maamuzi ya wengi (Majority)  hasa kwa ishu kubwa kama hii ya KATIBA MPYA! ni makosa makubwa hili tutalifananisha na swala la Gadafi kung'ang'ania madaraka pale nchini Libya .Maana kama katiba inanyima haki watu fulani na kuwapenndelea wachache wazidi kutugandamiza maana yake demokrasia hakuna!
         Swala la viongozi wakubwa serikalini kuhujumu serikali na wananchi kwa ujumla alafu wasichukuliwe hatua!  mbaya zaidi wanapambwa na kupewa pango wajifiche pia ni kitendo kibaya na cha kinyama kinachoitia doa serikali na imani ya wananchi kwa serikali kamwe haitapatikana hata kama serikali itavua ngozi yake yote ya mwili , mpaka pale wale wahalifu  wakishughulikiwa kwa hatua madhubuti tena waziwazi kuchukuliwa! 
       Lazima utambue kwamba ukiwa nje ya uwanja ni rahisi sana kulaumu na kumbeza mchezaji anapokosa goli, ukidai ungekua wewe ungeshinda! Pia ni rahisi kuruka ruka na kushangillia mchezaji anaposhinda pasipo kufikiria juhudi na maumivu aliyopata katika kushinda huko! 
      Ni lazima tukubaliane swala la kuongza nchi ni gumu sana, Viongozi wapaswa kuwa na  ushirikiano  katika kila hatua za  utendaji kazi wao serikalini na sio kubezana na kuzodoana kama watoto bungeni! wanabaki kugongagonga benchi wakivinadi vyama vyao wakati sisi wananchi wao tunamaisha magumu!
         Suala la la vyama lisipewe kipaumbele hata kidogo, wakiwa kwenye vikao vya serikali wafanye kazi kwa manufaa ya wananchi wanaowawakilisha.Tanzania bara tuige mfano wa Visiwani jamani!
Lengo ni kupata uongozi bora na sio chama bora, Washauriane na kutoa mapendekezo kwa lengo la kujenga na sio kukosoana! Maana hakuna mkamilifu duniani  kama ni suala la haki au sheria zipo njia nzuri za kuzungumza hadi tukafikia suluhu kuliko kulopoka kwenye halaiki Na kutupandikizia sumu!

         Watanzania sasa tumeamka Tunachagua Kiongozi bora na sio chama!       
         Mwisho namalizia kwa kusema ;-Serikali ya Tanzania kama imechaguliwa na wananchi na itekeleze matakwa ya wananchi wake. 
Viongozi wakiwa serikalini au bungeni waweke itikadi zao za chama na masilahi yao  pembeni.
Na wananchi Tuwe na mtizamo chanya juu ya serikali yetu na Tuache ghasia!   Maana Ghasia sio Demokrasia!          


                                   By S.E.MWITA 
                                                     Profesional Teacher 
                                        contact - phone :+255717010440 
              mail   :P.O.BOX 60080,DSM. 
              email : calmsam1@yahoo.com

No comments:

Post a Comment