Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake,
wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza
kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule
kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa
kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa
kushika ubao ulioelea majini akaanza kuelea nao,
maji yalimpeleka hadi kisiwa cha mbali sana
ambako hakukuwa na watu wala wanyama
isipokuwa wadudu tu! Alifika ufukweni amechoka
sana na asiyeamini tukio lililotokea, akaishi huko
kwa kula matunda. Aliweza kujenga ka-kibanda
kwa shida sana maana hakuwa na shoka wala
panga, hatimaye akaanza maisha mapya.
Aliishi muda mrefu kisiwani na tayari alishazoea
mazingira yale ya shida japo shida haizoeleki.
Mara zote nyakati za jioni aliwasha moto kwa
kupekecha vijiti. Siku moja kama kawaida yake
aliwasha moto nje karibu na kibanda chake, aliota
moto muda mrefu hatimaye akapitiwa na usingizi.
Alilala hapo hapo hadi usiku wa manane
aliposhtushwa na joto kali lisilo la kawaida.
Kumbe moto ulishika nyasi za kibanda chake na
kibanda chote kikaungua moto.Alilia sana na
kumlaani sana Mungu kwa mateso hayo akisema
"Hivi Mungu nimekukosea nini mpaka unitese
hivi? Pamoja na shida zote hizi bado
unaniongezea shida nyingine, umeteketeza makazi
yangu ilhali nimejenga kwa shida, Hukuridhika
kunitenga mbali na familia yangu nilipoishi kwa
raha? Hukuridhika kuwaua rafiki zangu wote
baharini? Kwanini Mungu umekuwa mkatili hivi?
Bora nife tuu maana nimeshachoshwa na hizi
shida!" akaendelea kulalamika na kumlaani Mungu
hadi kukapambazuka.
Ilipofika asubuhi aliiona meli ikija kwa mbali
kuelekea alipo, alishangaa maana hakuna meli
yoyote inayoweza kwenda kisiwa kile labda kama
imepotea njia. Meli ilipofika ufukweni yule kijana
akaifuata, alienda moja kwa moja hadi kwa
kapteni.Kapteni akamwambia "tuliona moto mkali
sana usiku tukahisi ni meli inawaka moto
tukasema tuje ili tutoe msaada..kwa kweli
tumetembea masaa mengi sana hadi kufika hapa,
mshukuru Mungu maana ametumia moto kutuleta
hapa" yule kijana kusikia hivyo alilia sana,
akajilaumu kwa jinsi alivyo mnung'unikia Mungu.
Akaelewa kuwa Mungu ana njia nyingi za kuleta
msaada kwa mtu. Akapiga magoti akatubu huku
akimshukuru Mungu. Safari ya kurudi nyumbani
ikaanza.
FUNDISHO: Wakati mwingine Kuna mambo
mabaya huwa yanatokea katika maisha yetu
yanayotufanya tuone kama Mungu ametusahau.
Tunamnung'unikia na kumlaumu Mungu bila
kujua kuwa Mungu ana njia nyingi sana kutuletea
msaada. Njia za Mungu huwa zinaonekana kama
ujinga fulani, lakini kiukweli ujinga wa Mungu
ndiyo akili kubwa ya mwisho ya mwanadamu.
Tunasahau kuwa mabaya tunayokutana nayo
yanafanya kazi kwa Manufaa ya hatma zetu.
Unaweza fukuzwa kazi usijue kumbe ndio
unaelekea katika kazi bora zaidi, unaweza
kuachwa na mtu uliyempenda sana ukadhani
ndiyo mwisho wa maisha kumbe Mungu
amekuandalia mtu mwingine mwenye mapenzi ya
dhati mtakayefikia malengo ya kujenga familia,
unaweza kukataliwa na kutengwa na ndugu
kumbe Mungu amekuandalia watu-baki
watakaofanikisha ufikie malengo yako pasipo
masimango ya ndugu, hata rafiki wanaweza
kukusaliti kumbe Mungu amewaondoa makusudi
ili kukuepusha na mabaya waliyoyapanga juu
yako. Sasa usimlaumu Mungu ukadhani
anakuzidishia matatizo, hapo anatafuta njia ya
kuyaondoa hayo matatizo.
Mshukuru Mungu kwa Kila Jambo, kwakuwa
hajawahi kukuwazia mabaya. Anakuwazia mema
sikuzote.
Tafadhari Share kama umeipenda na marafiki
zako wajifunze.
THE TRUTH
The people who do what let them live, Trust in God accepted JESUS as their personal savior, Satisfied on what they have, respect others help disabled and poor people, they are peace to any one. for give and forget is their system of life, To ask forgiveness is an easy task for them, even if its not their fault, hush and rude words never comes from their mouth even When they are angry, Ready to sacrifice their life for others..AND THIS IS HOW GOOD PEOPLE LIVE...
Friday, July 22, 2016
SOMA HII STORI UJIFUNZE KITU
Wednesday, July 13, 2016
MTU SAHIHI WA KUOLEWA AU KUMUOA
USIDANGANYIKE BINTI YANGU..!
Binti mmoja alitaka ushauri kutoka kwa Mwalimu na maongezi yao yalikuwa hivi.. :
🔹Binti : Shallom mwalimu..
🔹Mwl : Shallom maranatha, binti yangu.
🔹Binti : Mwl, kuna swali naomba nikuulize, maana linanisumbua sana kichwa changu.
🔹Mwl : usijal binti yangu, karibu.
🔹Binti : Mwl, mimi ni binti niliyeokoka na nampenda YESU, nina mchumba wangu ninampenda sana na yeye ananipenda pia, lakini yeye hajaokoka. Sasa ninaweza kuwa nae? Tuna malengo ya kuoana.
🔹Mwl : Binti yangu maandiko yanasema,
"Msifungiwe NIRA pamoja na wasioamini (msioane na watu wasiookoka), kwa jinsi isivyo sawasawa. Kwa maana pana Ushirika gani kati ya haki na Uasi? Tena pana shirika gani kati ya Nuru na Giza? Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye Asiyeamini? 2 wakorintho 6 :14-16.
Hivi binti yangu, mafuta unaweza ukachanganya na maji na vikakaa pamoja? Ingawa vyote ni vimiminika lakini haviwezi kukaa pamoja. Ni lazima vijitenge, mafuta yatakuwa juu na maji yatakaa chini.
🔹Binti : Lakini Mwl, si anaweza kubadilisha dini?
🔹Mwl : Binti yangu, wokovu si DINI, wokovu ni kuishi maisha matakatifu katika kristo Yesu, wokovu ni KUZALIWA kwa mara ya pili, wokovu ni NEEMA. I Petro 1 : 23, Yohana 3 : 5.
🔹Binti : Basi, Mwl nitamuhubiria aokoke..!
🔹Mwl : Kumuhubiria unaweza binti yangu, lakini sio kumfanya Aokoke, ni Mungu pekee ndiye mwenye uwezo huo. Usidanganyike binti yangu. Tena Yesu aliwaambia hivi Wayahudi :
"Akasema kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu Awezaye kuja kwangu (kuokoka) isipokuwa amejaliwa na Baba yangu " Yohana 6 : 65.
🔹Binti : Aah jamani, lakini si kuna andiko linasema mke kama hajaokoka atatakaswa na mumewe kama ameokoka na kama mume ndiye hajaokoka pia atatakaswa na mkewe aliyeokoka?
🔹Mwl : Kweli Mungu alikuwa sawa aliposema watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa (Hosea 4 :6). Binti yangu ni kweli kuna andiko hilo lakini halikuhusu wewe katika mazingira yako ya sasa.
Andiko hilo linawahusu watu waliofunga ndoa kabla hawajaokoka na baadaye mmoja wapo akawa ameokoka, hapo ndipo biblia inashauri kuwa yule aliyeokoka asimuache mwenzake kama atakuwa tayar kuendelea kuwa pamoja, maana yule asiyeokoka hutakaswa kupitia yule aliyeokoka ( 1 wakorintho 7 :12-16).
Hivyo si sawa kwa mtu aliyeokoka kutumia andiko hilo. Binti yangu, Usidanganyike.
🔹Binti : Lakini huyo kijana ananipenda kweli, yaan sijawah ona mwanaume anayenipenda kama yeye, yaan sijaona (kwa kusisitiza).
🔹Mwl : Hahaha, ni kweli binti yangu hakuna mwanaume anayekupenda zaidi yake? Je huyo mwanaume yupo tayar kufa kwa ajili yako? Sidhani binti yangu.
Lakini yupo mwanaume mmoja aliyekubali kufa kwa ajili yako, Yesu pekee ndiye aliyekubali kufa kwa ajili yako hakuna mtu mwingine ANAYEWEZA kufanya hivyo.
Maandiko yanasema : 'Bali alijeruhiwa (Yesu) kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu, Adhabu ya Amani yetu (mimi na wewe) ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake SISI tumepona' the Isaya 53 : 5.
🔹Binti :Lakini Mwl, mi siwez kumuacha yaan ninavyompenda, siwezi jaman.
🔹Mwl : Binti yangu, unawezaje kusema unampenda Yesu ikiwa huwezi kulitii neno lake? Yesu alisema mtu anayempenda hulitii Neno lake (Yohana 14 :23). Na pia alisema mtu asiyekubali kuviacha vitu vyote na kumfuata hawezi kuwa mwanafunzi wake (Luka 14 :33).
🔹Binti :Lakini Mwl, mbona sasa sioni vijana waliokoka wanaonipenda?
🔹Mwl : Binti, mambo ya rohoni hutambulika na kuonekana rohoni. Usitumie akili zako katika hili, ebu mwachie Mungu. 1 Wakorintho 2 : 14.
🔹Binti : Yaani hapa nilipo nimechoka sijui hata nifanyaje.
🔹Mwl : Maandiko yanasema, 'mwenye haki wangu ataishi kwa IMANI, Naye akisita-sita roho yangu haina furaha naye' Waebrania 10 : 38.
🔹Binti : sawa Mwl, nimeelewa.
🔹Mwl :Mungu AKUSAIDIE binti yangu, uwe mtendaji wa Neno na si msikiaji tu. Yakobo 1 : 21.
↪Hivyo ndivyo Maongezi yalivyokuwa kati ya Mwalimu na binti.
..................
Kuna msemo unasema.. :
"USIKUBALI KUMUACHA YESU KWA AJILI YA KITU CHOCHOTE KWA KUWA CHOCHOTE KINAWEZA KUKUACHA WAKATI WOWOTE ILA YESU ATAKUWA NA WEWE WAKATI WOTE KATIKA YOTE "
MUNGU AKUBARIKI..!
Tuesday, October 9, 2012
Wednesday, April 27, 2011
"Demokrasia sio Ghasia"
Wednesday, April 13, 2011
Tuesday, April 12, 2011
Teaching and learning Enviroment!

So
as to ensure Higher performance in school setting the Government and other organization deals with Education
must improve these environment of teaching and learning process
it involve
IN GOD I TRUST
Friday, April 8, 2011
Fight with target!
Life is Fighting! so you must fight harder with targets while knowing where you kick!